Moja kati ya
vitu vinavyowafanya vijana wengi washindwe kufurahia maisha yao ya kimahusiano
ni hali ya kwenda jino kwa jino na wapenzi wao. Vijana wengi wanajikuta kila
siku wakiingia katika matatizo na wenzi
wao kwa sababau hii.
Anataka ajue kila mpenzi wake anayewasiliana
naye,anataka kila safari ya mpenzi wake aifuatilie mpaka mwisho. Katika hali
hii ni lazima tu utajikuta ukiingia katika migogoro isiyo na lazima na mpenzi
wako.
Wakati wewe ukiona uko sahihi kwa msemo wa
abiria chunga mzigo wako, mwenzako ataona unafanya dunia isiwe mahala huru
kwake. Ndiyo, utakuwa unamnyima uhuru wake. Kuwa naye katika mahusiano haina
maana kuwa katengana na dunia nzima.
Nakubali kuwa inafaa awe na udhibiti wa kuwa
na wewe. Ajue tofauti ya sasa na zamani, ila pia jua ana marafiki na watu wake
wengine wakaribu hivyo ni lazima tu awe na mawasilaino nao. Huko katika shule
na kazini ni lazima tu alikuwa na watu muhimu wa kumsaidia katika masuala mbali
mbali ya kimaisha, sasa kuwa na wewe isiwe ndiyo mwisho wa urafiki wao. Suala
linalotakiwa hapo ni kuachana na wale tu wanaoonekana kama akiwa nao basi
mahusiano yenu kuwa imara ni ndoto za mchana. Unamjua mpenzi wako vizuri?
Kumjua vizuri mtu uliye naye itakupa fursa
ya kuwa na amani na kujikuta ukiwa mwenye furaha zaidi katika maisha yako.
Wengi hawawajui wapenzi wao. Kila wanachoambiwa ama kufanyiwa wao hufanya kuhisi na kujilazimisha kuamini. Hawana uhakika na
wapenzi wao!
Kila wanachofanyiwa wanahisi kwa sababau hawajui
vizuri wapenzi wao, na dhamira zao za
kuwa na wao. Wewe dhamira ya mpenzi wako unaijua?
Unajua
ni kwanini mpenzi wako kaamua kuwa na wewe? Ni kweli kwa sababu anakupenda au
ni kwa sababu hakuna aliyemfuata na kumwambia anampenda? Kuwa makini!
Wapenzi wengi wako katika mahusiano kwa sababu
tu hawana mahala pa kwenda. Wengine wapo katika mahusiano kwa kuwa kwao maisha
ni magumu hivyo wanatafuta sehemu ya kupatia unafuu wa maisha. Ukiwa na mtu wa
aina hiyo ni vyema kumpa msaada tu kisha kumuacha aendelee na hamsini zake, kwa
maana katu mtu wa aina hiyo hana furaha ya kimapenzi kuwa na wewe, na siku
mambo yake yakiwa poa tu ni lazima atajitoa katika ‘utumwa anaoutumikia kwako’.
Una
hakika unamjua mapenzi wako vizuri? Kweli umesoma macho yake nakugundua ‘I love
you’ yake inamaaisha kile kilichopo katika moyo wake? Mjue mpenzi wako ili uwe
na uhakika wa ahadi zenu mnazopanga pamoja.
Wengine wanapanga ahadi za kuishi milele na
wapenzi wao kumbe wenzao wanawatumia kama madaraja ya katika shida zao. Kwani we
hujawahi kusikia wakina f’lani wakisomesha alafu baadaye wakakimbiwa? Kwa ni
hujawahi kuona wanapendwa katika kipindi cha raha wakipata matatizo
wanakimbiwa? Hujawahi kuona? Mwenzio nimewahi!
Na
yote hii inasabababishwa kwa kutowajua vizuri wapenzi wao. Unafikiri kama ukimjua
vizuri mpenzi wako yote yatakutokea? Wapi!
Wakati yeye akijua yuko na zoba wa kupita,
wewe unamuona mjinga kwa kutojua kama umemjua. Wanaonung’unika leo na kulia
yasingewakuta hayo kama wangewajua wapenzi wao mapema. Wala usidhani kuwa ni
tabu. Si hivyo!
Anza kuwa makini na matendo ya mwenzako
kuanzia sasa. Acha kuchunguza katika namna isiyofaa. Mpe uhuru unaostahili
alafu kuwa makini na maneno na matendo yake kwako. Pia zingatia sana mahitaji
yake kwako. Je,yanalengo la kukomoa au kuna kitu kingine?
Wengi kutokana na mapenzi yao kwa wenzao
wamejikuta wakijitahidi kuwawatimizia mahitaji wanayoyataka wakidhani ni njia
ya kuonesha mapenzi yao kumbe wenzao wanawachukulia tofauti. Wanaowaona wajinga
wasiojua wanalofanya. Kuwa makini sana na mwenzako unaweza kumchukulia tofauti
bure. Unaweza kudhani si anayekufaa kumbe akawa ndiye mwenye uwezo wa kukufuta
machozi, au vinginevyo.
ramadhanimasenga@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni