Upo
katika muundo upi wa mapenzi? Wewe na mpenzi wako mahusiano yenu yakoje?
Niyafuraha na upendo au ni yale yanaokutegemea zaidi ili yawepo?
Ni ndoto ya kila mmoja kuwa katika mahusiano
yaliyotawaliwa na furaha na amani. Mahusiano yenye kila aina ya amani na
uchangamfu.
Ila kwa bahati mbaya ni wachache sana
walifanikiwa katika hilo. Wengi mahusiano yao ni kizungumkuti. Visa na maudhi
kwa kwenda mbele. Amani na upendo wamebaki kuvisikia kutoka kwa wengine, kwao
ni kitendawili. Wewe upo katika mahusiano ya namna gani?
Unaridhika na jinsi mapenzi wako alivyo
kwako. Japo huenda akawa hakupi fedha kutokana na sababu kadhaa lakini ni kweli
anaonesha kukujali? Anakupigia simu mara ngapi? Hata kama salio hana je, hata
kuku’beep’ tu inashindikana!
Je, wewe ndiyo kila siku umekuwa mwenye
kutaka kuonana naye huku yeye akiwa hana habari? Upo katika mapenzi ya namna
hiyo?
Mpenzi wako anakupa sababu yakufurahi au ndiyo
vile kila siku huwa unajutia uamuzi wa kuwa naye. Kila siku yeye kwako
anahitaji fedha ukiacha kumpa basi humpendi. Je, mpenzi wako ni wa aina hiyo?
Jamani, tunapaswa kuelewa kuwa mapenzi ni raha
na faraja sana. Unapokuwa hauko katika mapenzi ya namna hiyo unapaswa kujiuliza
Hapo huenda ukawa umedondokea katika mikono
ya wasanii wa mapenzi. Ambao wao kwao mapenzi huwa na misimu kama ligi za
mpira. Leo anaweza kujifanya anakupenda sana ila kesho hata ‘sms’ yako hajibu.
Na akijibu basi ni kwa maneno ya mkato mno. Kama siyo ‘thanks, basi itakuwa ‘poa
tu’. Ni vyema ukajiuliza muundo wa mapenzi uliyopo ili kuweza kuchukua hatua
zinazofaa kabla mambo hayajazidi kuharibika zaidi.
Kuwa na mpenzi ambaye hakupi raha na furaha
ni kupoteza muda tu na kujipa ‘stress’ za bure. Ni wewe ambaye kila siku
umekuwa ukilia tu. Ni wewe ambaye kila siku unaomba msamaha kwa makosa ambaye
anakufanyia wewe.Hayo mapenzi kweli?
Kulilia penzi la mtu asiyeonesha kukujali
wala kutambua thamani yako ni kujiingiza katika utumwa. Utumwa ambao mwisho
wake nikukuachia majuto makuu ya kukaa kwa muda mrefu katika mahusiano na mtu
ambaye mwisho wenu utakuwa ni ule ambao hukuutegeamea. Mwisho wa kutengana
haliyakuwa huku ukiwa amekupotezea muda pengine na thamani yako machone pa
wengi.
Yangalie vizuri matendo yake juu yako.
Angalia maneno yake. Je, yanakufanya ufurahi? Ni matendo ya wapendanao?
Maisha yako yanahitaji furaha ili uweze
kuishi kwa amani. Na asilimia kubwa ya furaha inatakiwa kusababishwa na mpenzi
wako. Sasa vipi unapokuwa katika mahusiano na mtu anayekukera na kukufanya
ujute? Kweli utakuwa na furaha? Ni kitendawili. Kama si kuambulia msongo wa
mawazo pamoja na sura kukunjika kwa hasira za kila siku!
Kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hapendi
kukuona na furaha ni kujimaliza. Kwa sababu atafanya utendaji wako wa kazi
kushuka,uchangamfu ukupotee kutokana na karaha zake. Ni ngumu mno kupata hata
maendeleo kama huwi mtu wa furaha na uchangamfu. Na pia ni ngumu sana kuwa mtu
wa furaha kama uko katika mahusiano na mtu wa vituko na visa visivyo kwisha.
Kila siku unamwambia neno moja. Kila siku
wewe ndiye unamtafuta. Chunguza vizuri mahusiano yako. Kisha jibu swali hili,
Upo katika mahusiano ya namna gani?
ramadhanimasenga@yahoo.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni