Ili mapenzi
yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona
thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini
wala humjali.
Muunganiko
wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka
sisi.
Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana
halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika
kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani.
Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele.
Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.
Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye
hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika
utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe
maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale
mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.
Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya
kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana
mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye
hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si
yeye.
Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule
mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana
na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu
msichana.
Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza
kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza
msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa
naye hivyo hivyo.
Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa.
Kweli walikuwa pamoja. Ila unajua
kinachomkuta sasa?
Kila jamaa anapogombana na yule msichana
mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila
kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo
itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.
Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma
wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona
haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila
siku kwa kumuangalia yeye tu?
Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na
unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia
na wewe sasa.
Ona
thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu
asiyeona thamani yako.
Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani,
bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali
na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa
mapenzi kwa kuiona thamani yako.
Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana
unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au
muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.
Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau
shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala
afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno
mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema
wapendwa.
ramadhanimasenga@yahoo.com
Playtech Launches The Best New Slots By Casino Apps in 2021
JibuFutaThe best 경상남도 출장마사지 new slots 대전광역 출장마사지 machines by 순천 출장샵 Playtech include 사천 출장안마 The Best New Slots By Casino Apps in 2021 · Top New Slots by 충주 출장안마 Playtech: Top Slots Games